< 1 Wafalme 3 >

1 Solomoni akafanya urafiki na Mfalme Farao wa Misri na kumwoa binti yake. Akamleta huyo binti katika Mji wa Daudi mpaka alipomaliza kujenga jumba lake la kifalme na Hekalu la Bwana, pamoja na ukuta kuzunguka Yerusalemu.
And Solomon became the son-in-law of Pharaoh king of Egypt, and took Pharaoh's daughter, and brought her into the City of David, until he had made an end of building his own house, and the house of the LORD, and the wall of Jerusalem all around.
2 Hata hivyo, watu bado walikuwa wakitoa dhabihu huko kwenye vilima, kwa sababu Hekalu lilikuwa bado halijajengwa kwa ajili ya Jina la Bwana.
Only the people sacrificed in the high places, because there was no house built for the name of the LORD until those days.
3 Solomoni akaonyesha upendo wake kwa Bwana kwa kuenenda sawasawa na amri za Daudi baba yake, ila yeye alitoa dhabihu na kufukiza uvumba huko mahali pa juu.
Solomon loved the LORD, walking in the statutes of David his father: only he sacrificed and burnt incense in the high places.
4 Mfalme akaenda Gibeoni kutoa dhabihu, kwa maana ndipo palipokuwa mahali pa juu pa kuabudia, naye Solomoni akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya hayo madhabahu.
The king went to Gibeon to sacrifice there; for that was the great high place. Solomon offered a thousand burnt offerings on that altar.
5 Bwana akamtokea Solomoni huko Gibeoni wakati wa usiku katika ndoto, naye Mungu akasema, “Omba lolote utakalo nikupe.”
In Gibeon the LORD appeared to Solomon in a dream by night; and God said, "Ask what I shall give you."
6 Solomoni akajibu, “Umemfanyia mtumishi wako, baba yangu Daudi, fadhili nyingi, kwa kuwa alikuwa mwaminifu kwako na mwenye haki, tena mnyofu wa moyo. Nawe umemzidishia fadhili hii kuu kwani umempa mwana wa kuketi kwenye kiti chake cha ufalme, kama ilivyo leo.
Solomon said, "You have shown to your servant David my father great loving kindness, according as he walked before you in truth, and in righteousness, and in uprightness of heart with you. You have kept for him this great loving kindness, that you have given him a son to sit on his throne, as it is this day.
7 “Sasa, Ee Bwana Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako mfalme badala ya baba yangu Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu, wala sijui jinsi ya kutekeleza wajibu wangu.
Now, LORD my God, you have made your servant king instead of David my father. I am but a little child. I do not know how to go out or come in.
8 Mtumishi wako yuko hapa miongoni mwa watu uliowachagua: taifa kubwa, watu wengi wasioweza kuhesabika wala kutoa idadi yao.
Your servant is in the midst of your people which you have chosen, a great people, that can't be numbered nor counted for multitude.
9 Hivyo mpe mtumishi wako moyo wa ufahamu ili kutawala watu wako na kupambanua kati ya mema na mabaya. Kwa maana, ni nani awezaye kutawala watu wako hawa walio wengi hivi?”
Give your servant therefore an understanding heart to judge your people, that I may discern between good and evil; for who is able to judge this your great people?"
10 Bwana akapendezwa kwamba Solomoni ameliomba jambo hili.
The speech pleased the LORD, that Solomon had asked this thing.
11 Basi Mungu akamwambia, “Kwa kuwa umeomba neno hili na hukuomba maisha marefu au upate utajiri kwa nafsi yako, wala adui zako wafe, bali umeomba ufahamu katika kutoa haki,
God said to him, "Because you have asked this thing, and have not asked for yourself long life, neither have asked riches for yourself, nor have asked the life of your enemies, but have asked for yourself understanding to discern justice;
12 nitafanya lile uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwepo mtu mwingine kama wewe, wala kamwe hatakuwepo baada yako.
look, I have done according to your word. Look, I have given you a wise and an understanding heart; so that there has been none like you before you, neither after you shall any arise like you.
13 Zaidi ya hayo, nitakupa yale ambayo hukuomba, yaani utajiri na heshima, ili kwamba maisha yako yote hapatakuwa na mtu kama wewe miongoni mwa wafalme.
I have also given you that which you have not asked, both riches and honor, so that there shall not be any among the kings like you, all your days.
14 Nawe kama ukienenda katika njia zangu na kutii sheria na amri zangu kama baba yako Daudi alivyofanya, nitakupa maisha marefu.”
If you will walk in my ways, to keep my statutes and my commandments, as your father David walked, then I will lengthen your days."
15 Ndipo Solomoni akaamka, akatambua kuwa ilikuwa ndoto. Akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya Sanduku la Agano la Bwana, naye akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha akawafanyia watumishi wake wote karamu.
Solomon awoke; and look, it was a dream. Then he arose and came to Jerusalem, and stood before the ark of the covenant of the LORD, and offered up burnt offerings, offered peace offerings, and made a feast for all his servants.
16 Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake.
Then two women who were prostitutes came to the king, and stood before him.
17 Mmojawapo akasema, “Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunaishi kwenye nyumba moja. Nilikuwa nimezaa alipokuwa pamoja nami.
The one woman said, "Oh, my lord, I and this woman dwell in one house. I delivered a child with her in the house.
18 Siku ya tatu baada ya mtoto wangu kuzaliwa, mwanamke huyu pia naye akazaa mtoto. Tulikuwa peke yetu, hapakuwa na mtu mwingine yeyote katika nyumba isipokuwa sisi wawili.
It happened the third day after I delivered, that this woman delivered also. We were together. There was no stranger with us in the house, just us two in the house.
19 “Wakati wa usiku mwana wa huyu mwanamke akafa kwa sababu alimlalia.
This woman's child died in the night, because she lay on it.
20 Hivyo akaondoka katikati ya usiku na kumchukua mwanangu kutoka ubavuni pangu wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa nimelala. Akamweka kifuani mwake na kumweka mwanawe aliyekufa kifuani mwangu.
She arose at midnight, and took my son from beside me, while your handmaid slept, and laid it in her bosom, and laid her dead child in my bosom.
21 Asubuhi yake, nikaamka ili kumnyonyesha mwanangu, naye alikuwa amekufa! Lakini nilipomwangalia sana katika nuru ya asubuhi, niliona kuwa hakuwa yule mwana niliyekuwa nimemzaa.”
When I rose in the morning to nurse my child, look, it was dead; but when I had looked at it in the morning, look, it was not my son, whom I bore."
22 Huyo mwanamke mwingine akasema, “Hapana! Mwana aliye hai ndiye wangu, aliyekufa ni wako.” Lakini yule wa kwanza akasisitiza, “Hapana! Mwana aliyekufa ni wako, aliye hai ni wangu.” Hivi ndivyo walivyobishana mbele ya mfalme.
The other woman said, "No; but the living is my son, and the dead is your son." This said, "No; but the dead is your son, and the living is my son." Thus they spoke before the king.
23 Mfalme akasema, “Huyu anasema, ‘Mwanangu ndiye aliye hai, na aliyekufa ndiye mwanao,’ maadamu yule anasema, ‘Hapana! Aliyekufa ni wako, na aliye hai ni wangu.’”
Then the king said, "The one says, 'This is my son who lives, and your son is the dead;' and the other says, 'No; but your son is the dead one, and my son is the living one.'"
24 Kisha mfalme akasema, “Nileteeni upanga.” Basi wakamletea mfalme upanga.
The king said, "Get me a sword." They brought a sword before the king.
25 Ndipo mfalme akatoa amri: “Mkate mtoto aliye hai vipande viwili; mpe huyu nusu na mwingine nusu.”
The king said, "Divide the living child in two, and give half to the one, and half to the other."
26 Mwanamke ambaye mwanawe alikuwa hai akajawa na huruma kwa ajili ya mwanawe na kumwambia mfalme, “Tafadhali, bwana wangu, mpe yeye mtoto aliye hai! Usimuue!” Lakini yule mwanamke mwingine akasema, “Mkate vipande viwili. Asiwe wangu au wake!”
Then the woman whose the living child was spoke to the king, for her heart yearned over her son, and she said, "Oh, my lord, give her the living child, and in no way kill it." But the other said, "It shall be neither mine nor yours. Divide it."
27 Kisha mfalme akatoa uamuzi wake: “Mpeni mama wa kwanza mtoto aliye hai. Msimuue; ndiye mama yake.”
Then the king answered, "Give her the living child, and in no way kill it. She is its mother."
28 Wakati Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki.
All Israel heard of the judgment which the king had judged; and they feared the king: for they saw that the wisdom of God was in him, to do justice.

< 1 Wafalme 3 >