< 1 Nyakati 8 >

1 Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza, Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu,
Benjamin engendra Béla, son premier-né, Ashbel le second, Achrach le troisième,
2 Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.
Nocha le quatrième, et Rapha le cinquième.
3 Wana wa Bela walikuwa: Adari, Gera, Abihudi,
Les fils de Béla furent: Addar, Guéra, Abihud,
4 Abishua, Naamani, Ahoa,
Abishua, Naaman, Achoach,
5 Gera, Shefufani na Huramu.
Guéra, Shéphuphan et Huram.
6 Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:
Voici les enfants d'Échud; ils étaient chefs des maisons des pères des habitants de Guéba, et ils les transportèrent à Manachath:
7 Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni.
Naaman, Achija et Guéra; c'est lui qui les transporta. Il engendra Uzza et Achichud.
8 Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara.
Shacharaïm eut des enfants au pays de Moab, après qu'il eut renvoyé Hushim et Baara, ses femmes.
9 Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu,
Il engendra de Hodèsh, sa femme, Jobab, Tsibia, Mésha, Malcam,
10 Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao.
Jéuts, Shocja et Mirma. Ce sont là ses fils, chefs des pères.
11 Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.
De Hushim il engendra Abitub, et Elpaal.
12 Wana wa Elpaali walikuwa: Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka),
Les fils d'Elpaal: Éber, Misheam, et Shémer, qui bâtit Ono, Lod et les villes de son ressort.
13 na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.
Béria et Shéma, qui étaient chefs des pères des habitants d'Ajalon, mirent en fuite les habitants de Gath.
14 Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi,
Achio, Shashak, Jérémoth,
15 Zebadia, Aradi, Ederi,
Zébadia, Arad, Éder,
16 Mikaeli, Ishpa, na Yoha.
Micaël, Jishpha et Jocha, étaient fils de Béria.
17 Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi,
Zébadia, Meshullam, Hizki, Héber,
18 Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali.
Jishméraï, Jizlia, et Jobab, étaient fils d'Elpaal.
19 Yakimu, Zikri, Zabdi,
Jakim, Zicri, Zabdi,
20 Elienai, Silethai, Elieli,
Éliénaï, Tsilethaï, Éliel,
21 Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.
Adaja, Béraja, et Shimrath, étaient fils de Shimeï.
22 Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli,
Jishpan, Éber, Éliel,
23 Abdoni, Zikri, Hanani,
Abdon, Zicri, Hanan,
24 Hanania, Elamu, Anthothiya,
Hanania, Élam, Anthothija,
25 Ifdeya na Penueli.
Jiphdéja et Pénuel, étaient fils de Shashak.
26 Shamsherai, Sheharia, Athalia,
Shamshéraï, Shécharia, Athalia,
27 Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
Jaareshia, Élija et Zicri, étaient fils de Jérocham.
28 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.
Ce sont là les chefs des maisons des pères, chefs selon leur naissance. Ils habitaient à Jérusalem.
29 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni. Mke wake aliitwa Maaka.
Le père de Gabaon habitait à Gabaon; sa femme s'appelait Maaca.
30 Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,
Son fils, le premier-né, fut Abdon; puis Tsur, Kis, Baal, Nadab,
31 Gedori, Ahio, Zekeri,
Guédor, Achio et Zéker.
32 na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
Mikloth engendra Shiméa. Ils habitèrent aussi près de leurs frères à Jérusalem, avec leurs frères.
33 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.
Ner engendra Kis; Kis engendra Saül; Saül engendra Jonathan, Malkishua, Abinadab et Eshbaal.
34 Yonathani akamzaa: Merib-Baali, naye Merib-Baali akamzaa Mika.
Fils de Jonathan: Mérib-Baal. Mérib-Baal engendra Mica.
35 Wana wa Mika walikuwa: Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi.
Fils de Mica: Pithon, Mélec, Thaeréa et Achaz.
36 Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa.
Achaz engendra Jéhoadda; Jéhoadda engendra Alémeth, Azmaveth et Zimri; Zimri engendra Motsa;
37 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.
Motsa engendra Binea, qui eut pour fils Rapha, qui eut pour fils Éleasa, qui eut pour fils Atsel.
38 Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao: Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli.
Atsel eut six fils, dont voici les noms: Azrikam, Bocru, Ismaël, Shéaria, Obadia et Hanan. Tous ceux-là étaient fils d'Atsel.
39 Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa: Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti.
Fils d'Eshek, son frère: Ulam, son premier-né, Jéush le second, et Éliphélet le troisième.
40 Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150. Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.
Les fils d'Ulam furent de vaillants guerriers, tirant de l'arc; et ils eurent beaucoup de fils et de petits-fils, cent cinquante. Tous ceux-là sont des enfants de Benjamin.

< 1 Nyakati 8 >