< Luka 4 >

1 Boka po, Yesu abile atwalilwe Roho Mpeletau, atibuya boka kubende Jordani, ni ationgozwa ni Roho mu'lijangwa
Kisha, Yesu akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Mto Jordani, na aliongozwa na Roho jangwani
2 kwa machoba arobaini, ni kwoo atijaribiwa ni nchela. Muda woo alile kwaa chochote, ni mwishowe wa muda uno ayiisile njala.
kwa siku arobaini, na huko alijaribiwa na Ibilisi. Wakati huo hakula chochote, na mwisho wa wakati huo alihisi njaa.
3 Nchela atikum'bakia, “kama wenga ywa mwana wa Nnongo, liamuru liwe leno lipangite nkate.”
Ibilisi akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, liamru jiwe hili kuwa mkate.”
4 Yesu kaayangwa, itiandikwa; mundu atama kwaa nkate kichake.”
Yesu akamjibu, “Imeandikwa; 'mtu hataishi kwa mkate pekee.”
5 Boka po nchela atikumuongoza kunani kwenye kilele sa kitombe, na atikumlaya falme yoti pakilambo kwa muda mfupi.
Kisha Ibilisi alimwongoza juu kwenye kilele cha mlima, na akamwonyesha falme zote za dunia kwa muda mfupi.
6 Nchela atikum'bakiya, “Nipala kukupatia mamlaka ya tawala falme yeno yoti pamope na fahari yake. Niwecha kukupanga nya kwa sababu nyoti nitikabidhiwa kwango niitawale na nindawecha kumpeya yoyoti nimpalae kumpeya.
Ibilisi akamwambia, “Nitakupa mamlaka ya kutawala falme hizi zote pamoja na fahari zake. Naweza kufanya hivyo kwa sababu vyote vimekabidhiwa kwangu nivitawale, na ninaweza kumpa yeyote nitakaye kumpa.
7 Kwa nyo, kati unda niaminia na kuniabudu, vitu vino vyooti vipala panga vyako.”
Kwahiyo, kama utaniinamia na kuniabudu, vitu hivi vyote vitakuwa vyako.”
8 Lakini Yesu kan'yangwa ni kummakiya, “iandikilwe,” Lazima umwabudu Ngwana Nnongo wako, ni lazima umtumikie ywembe kichake.”
Lakini Yesu alijibu na kumwambia, “Imeandikwa, “lazima umwabudu Bwana Mungu wako, na lazima umtumikie Yeye peke yake.”
9 Baadaye nchela atikumuangoza Yesu hadi ku'Yerusalem ni kum'beka sehem ya kunani kabisa ya jengo lya hekalu ni kum'bakia, “Kati wenga ni mwana wa Nnongo, ujitombwe pae boka pano.
Baadaye Ibilisi alimwongoza Yesu hadi Yerusalemu na kumweka sehemu ya juu kabisa ya jengo la hekalu na kumwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa.
10 “Kwasababu iandikilwe “Apala lagiya malaika bake bakutunze ni kukulenda,
Kwa sababu imeandikwa, “Atawaagiza malaika zake wakutunze na kukulinda,
11 na bapala kukukakatuya kunani muluboko lyake ili kwamba kana ulumi magolo gako kunani ya liwe.”
na watakuinua juu mikononi mwao ili kwamba usiumize miguu yako juu ya jiwe.”
12 Yesu atikumjibu akim'bakia, “Itinenwa, “kana umjaribu Ngwana Nnongo wako.”
Yesu akijibu alimwambia, “Imenenwa, “usimjaribu Bwana Mungu wako.”
13 Nchela payomwile kumjaribu Yesu atiboka ni kumleka hadi muda wenge.
Ibilisi alipomaliza kumjaribu Yesu, alienda zake na kumwacha hadi wakati mwingine.
14 Boka po Yesu atibuya Galilaya kwa ngupu za Roho, ni habari kumhusu ywembe zitienea ni sambaa katika mikoa yapapipi yoti.
Kisha Yesu alirudi Galilaya kwa nguvu za Roho, na habari kumhusu yeye zikaenea na kusambaa katika mikoa jirani yote.
15 Atifundisha katika masinagogi yabe, ni kila yumo atikumsifu.
Alifundisha katika masinagogi yao, na kila mmoja alimsifu.
16 Lichoba limo ayei Nazareti, mji ambao atilekwa na kla. Kati cha ibile desturi yake atijingya ku'lisinagogi lichoba lya sabato, ni atiyema soma liandiko.
Siku moja alikwenda Nazareti, mji ambao alilelewa na kukulia. Kama ilivyokuwa desturi yake aliingia kwenye sinagogi siku ya sabato, na alisimama kusoma maandiko.
17 Atikabidhiwa gombo lya nabii Isaya nyoo, atiundwa gombo na pala sehemu yaiandikilwe,
Alikabidhiwa gombo la nabii Isaya, hivyo, alilifungua gombo na akatafuta sehemu iliyoandikwa,
18 Roho wa Ngwana ywa mnani yango, keasababu anijeile mauta hubiri habari njema kwa maskini. Atikunituma tangaza uhuru kwa wafungwa ni panga bababona kwaa wecha bona kae kubabeka huru balo baba kandamizwa,
“Roho wa Bwana yuu juu yangu, kwa sababu alinitia mafuta kuhubiri habari njema kwa maskini. Amenituma kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kuwafanya wasioona waweze kuona tena. Kuwaweka huru wale wanaogandamizwa,
19 tangaza mwaka ambao Ngwana apala laga wema wake.”
kuutangaza mwaka ambao Bwana ataonesha wema wake.”
20 Boka po po akalitaba gombo, atikumrudishia kiongozi wa sinagogi, ni tama pae minyo ya bandu boti babile mu'lisinagogi bati kumlinga yembe.
Kisha akalifunga gombo, akamrudishia kiongozi wa sinagogi, na akaketi chini. Macho ya watu wote waliokuwa katika sinagogi yalimwangalia yeye.
21 Atumbwile longela nakwe akibaya, “Leno andiko lino litimile mmasikio yinu.
Alianza kuzungumza nao akisema, “Leo andiko hili limetimizwa masikioni mwenu.”
22 Kila yumo palo atishuhudia chelo cha kibaite, Yesu, ni benge miongoni mwabe batishangala na maneno ga hekima gagabile bokya katika nkano wake, Babile bakibaya, yono ni kijana tu wa Yusufu, nyonyo kwa?”
Kila mmoja pale alishuhudia kile alichokisema Yesu, na wengi miongoni mwao walishangazwa na maneno ya hekima yaliyokuwa yakitoka katika kinywa chake. Walikuwa wakisema, “huyu ni kijana tu wa Yusufu, siyo hivyo?”
23 Yesu atikubabakiya, “hakika mpala baya methal ino kwango nee,'”N'ganga jiponye mwene, choti chatuyowine panga Kapernaumu, mukipange pano kae kukaya kwinu.'”
Yesu akawaambia, “hakika mtasema methali hii kwangu, “Tabibu, jiponye mwenyewe. Chochote tulichosikia ukifanya Kapernaumu, kifanye hapa pia kijijini kwako.”
24 Kae abayite, “hakika nindakuwabakiya mwenga, ndopo nabii angayeketilwa kachake.”
Pia alisema, “hakika nawaambia ninyi, hakuna nabii anayekubalika katika nchi yake.”
25 Lakini nindakuwabakiya mwenga kweli kwamba kwabile ni bawelikwe banambone Israel katika kipindi sa Eliya, muda kunani paitabilwe ntopo na ula kwa miaka itatu ni nusu, muda kwabile ni ndele ngolo pa'kilambo choti.
Lakini nawaambia ninyi kweli kwamba kulikuwa na wajane wengi Israel katika kipindi cha Eliya, wakati mbingu ilipofungwa kusiwe na nvua kwa miaka mitatu na nusu, wakati kulipokuwa na njaa kubwa katika nchi yote.
26 Lakini Eliya atumwile kwa yeyote yumo kwabe, lakini kwa mjane yumo ywa tamile Sarepta papipii ni mjo wa Sidoni.
Lakini Eliya hakutumwa kwa yeyote mmoja wao, lakini kwa mjane mmoja tu aliyeishi Sarepta karibu na mji wa Sidoni.
27 Pia kwabile ni hakomo banambone Israel katika kipinda sa Elisha nabii, lakini ntopo hata yumowabe yapomwile isipokuwa Naamani mundu wa Siria.
Pia, kulikuwa na wakoma wengi Israel katika kipindi cha Elisha nabii, lakini hakuna hatammoja wao aliyeponywa isipokuwa Naamani mtu wa Siria.
28 Bandu boti nkati ya sinagogi batwele ni gadhabu payowine haga goti.
Watu wote ndani ya sinagogi walijawa na gadhabu walipoyasikia haya yote.
29 Batiyema ni batikunchukuma panja ya mji, ni kumwongocha mpaka mu'mbwegu ya kitombe sa mji ambapo mji wabe wachengitwe kunani yake, ili waweche kumtomboya pae.
Walisimama na kumsukumizia nje ya mji, na kumwongoza mpaka kwenye ukingo wa mlima wa mji ambapo mji wao ulijengwa juu yake, ili waweze kumtupa chini.
30 Lakini apitile salama nkati yabe ni yendya zake.
Lakini alipita salama katikati yao na akaenda zake.
31 Boka po atiyelya Kapernaumu, katika mji wa Galilaya. Sabato yimo abile atifundisha bandu nkati ya sinagogi.
Kisha alitelemkia Kapernaumu, katika mji wa Galilaya. Sabato moja alikuwa akifundisha watu ndani ya sinagogi.
32 Batishangala ni mapundisho gake, kwasababu atifundisha kwa mamlaka.
Walishangazwa na mafundisho yake, kwasababu alifundisha kwa mamlaka.
33 Nambeambe lichoba liyo nkati a sinagogi, kwabile ni mundu abile ni roho nchafu wa nchela, ni atilela kwa lilobe la kunani,
Sasa siku hiyo ndani ya sinagogi, kulikuwa na mtu aliyekuwa na roho ya pepo mchafu, na alilia kwa sauti ya juu,
34 “Tubi ni namani nakwe, Yesu wa Nazareti? Uichile kutuyomwa? Nitangite wenga wa nyai! Wenga wa mpeetau wa Nnongo!”
“Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninajua wewe ni nani! Wewe ni mtakatifu wa Mungu!”
35 Yesu atikumkemeya nchela buya, “ukotoke liki, ni u'mboke mundu yuno! Nchela yolo atikumtaikwa mundu yolo pae nkati yabe, atikum'boka yolo mundu bila ya kumsababishia maumivu gogoti.
Yesu alimkemea pepo akisema, “Nyamaza kimya, na umtoke mtu huyu!” Pepo yule alipomtupa mtu yule chini katikati yao, alimtoka yule mtu bila ya kumsababishia maumivu yoyote.
36 Bandu boti batishangala, ni endelea kulongela kikowe chelo kila yumo nanyine, batibaya, “ni makowe ga aina gani haga?”Atikubaamuru roho bachapu kwa mamlaka ni ngupu ni bapala boka.
Watu wote walishangaa, na waliendelea kuzungumzia jambo hilo kila mmoja na mwenzake. Wakasema, “Ni maneno ya aina gani haya?” Anawaamuru roho wachafu kwa mamlaka na nguvu na watondoka.”
37 Nga nyo, habari kunani ya esu itienea katika makowe gabazunguka mkoa wono.
Hivyo, habari juu ya Yesu zilienea kila sehemu katika maeneo yanayozunguka mkoa huo.
38 Boka po Yesu atiboka katika mji wolo ni atijingia katika nyumba ya Simoni. Nambeambe, mao bake mkwe ni Simoni abile andaminya homa kali, ni batikumsihi kwa niaba yake.
Kisha Yesu aliondoka katika mji huo na akaingia katika nyumba ya Simoni. Sasa, mama mkwe wake na Simoni alikuwa anaumwa homa kali, na wakamsihi kwa niaba yake.
39 Nga nyo, Yesu atiegelelya, atikemea ile homa ni itikumleka ghafla atiyema ni tumbwa kubatumikiya.
Hivyo, Yesu alimsogelea, akaikemea ile homa na ikamwachia. Ghafla alisimama na akaanza kuwatumikia.
40 Liumu laitimbweli yima, bandu katika batimletea Yesu kila yumo ywabile atama ni maradhi ya aina ganambone abekite luboko lwake kunani ya kila mtamwe ni atikubaponya boti.
Jua lilipokuwa likizama, watu walimletea Yesu kila mmoja aliyekuwa mgonjwa wa maradhi ya aina mbalimbali. Aliweka mikono yake juu ya kila mgonjwa na akawaponya wote.
41 Ni nchela kae yatikuwapiya banambone wabe bakilela kwa malobe ni baya, “wenga ni mwana wa Nnongo! Yesu atikuwakemeia mashetani ni atikubaruhusu balongele, kwa sababu batitanga kwamba ywembe abile ni kristo.
Mapepo pia yaliwatoka wengi wao yakilia kwa sauti na kusema, “Wewe ni mwana wa Mungu!” Yesu aliwakemea mapepo na hakuwaruhusu waongee, kwa sababu walijua kwamba yeye alikuwa ni Kristo.
42 Muda pauyomwike, ayei eneo labile ntopo mundu. Makutano ga bandu babile bakimpala na icha katika eneo lya abile. Batijaribu kunkanikiya kana ayende kulipire nakwe.
Wakati kulipopambazuka, alienda eneo lisilokuwa na watu. Makutano ya watu walikuwa wakimtafuta na wakaja katika eneo alilokuwapo. Walijaribu kumzuia asiende mbali na wao.
43 Lakini atikuwabakiya, “Lazima pia nihubiri habari inanoga ya ufalme wa Nnongo katika miji yenge yanambone, kwa kuwa yeno nga sababu nititumwa pano.
Lakini akawaambia, “Lazima pia nihubiri habari njema za ufalme wa Mungu katika miji mingine mingi, kwa kuwa hii ndiyo sababu nilitumwa hapa.”
44 “Boka po atiyendelea hubiri nkati ya masinagogi katika uyahudi woti.
Kisha aliendelea kuhubiri ndani ya masinagogi katika uyahudi wote.

< Luka 4 >