< Philippians 3 >

1 Finally, my brothers, rejoice in the Lord! To write the same things to you, to me indeed is not tiresome, but for you it is safe.
Hatimaye, ndugu zangu furahini katika Bwana. Sioni usumbufu kuwaandikia tena maneno yaleyale. Haya mambo yatawapa usalama.
2 Beware of the dogs; beware of the evil workers; beware of the false circumcision.
Jihadharini na mbwa. Jihadharini na watenda kazi wabaya. Jihadharini na wale wajikatao miili yao.
3 For we are the circumcision, who worship God in the Spirit, and rejoice in Christ Jesus, and have no confidence in the flesh;
Kwa kuwa sisi nndiyo tohara. Sisi ndiyo huwa tumwabudu Mungu kwa msaada wa Roho. Tujivuniao katika Kristo Yesu, na ambao hatuna ujasiri katika mwili.
4 though I myself might have confidence even in the flesh. If any other man thinks that he has confidence in the flesh, I yet more:
Hata hivyo, kama kungekuwa na mtu wa kuutumainia mwili huu, mimi ningeweza kufanya hivyo zaidi.
5 circumcised the eighth day, of the stock of Israel, of the tribe of Benjamin, a Hebrew of Hebrews; concerning the law, a Pharisee;
Kwani nilitahiriwa siku ya nane, nilizaliwa katika kabila la Waisraeli. Ni wa kabila la Benjamini. Ni Mwebrania wa waebrani. Katika kuitimiza haki ya sheria ya Musa, nilikuwa, Farisayo.
6 concerning zeal, persecuting the assembly; concerning the righteousness which is in the law, found blameless.
Kwa juhudi zangu nililitesa Kanisa. Kwa tuitii haki ya sheria, sikuwa na lawama kisheria.
7 However, I consider those things that were gain to me as a loss for Christ.
Lakini katika mambo yote niliyoyaona kuwa ya faida kwangu mimi, niliyahesabu kama takataka kwa sababu ya kumfahamu Kristo.
8 Yes most certainly, and I count all things to be a loss for the excellency of the knowledge of Christ Jesus, my Lord, for whom I suffered the loss of all things, and count them nothing but refuse, that I may gain Christ
Kwa kweli, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kutokana ubora wa kumjua wa Kristo Yesu Bwana wangu. Kwa ajili yake nimeaacha mambo yote, nayahesabu kama takataka ili nimpate Kristo
9 and be found in him, not having a righteousness of my own, that which is of the law, but that which is through faith in Christ, the righteousness which is from God by faith,
na nionekane ndani yake. Sina haki yangu binafisi kutoka katika sheria, bali ninayo haki ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, itokayo kwa Mungu, yenye msingi katika imani.
10 that I may know him and the power of his resurrection, and the fellowship of his sufferings, becoming conformed to his death,
Sasa nataka kumfahamu yeye na nguvu ya ufufuo wake na ushirika wa mateso yake. Nataka kubadilishwa na Kristo katika mfano wa kifo chake,
11 if by any means I may attain to the resurrection from the dead.
angalau niweze kuwa na matumaini katika ufufuo wa wafu.
12 Not that I have already obtained, or am already made perfect; but I press on, that I may take hold of that for which also I was taken hold of by Christ Jesus.
Siyo kweli kwamba tayari nimeishayapata mambo hayo, au kwamba nimekuwa mkamilifu katika hayo. Bali najitahidi ili niweze kupata kile kupata kile nilichopatikana na Kristo Yesu.
13 Brothers, I don’t regard myself as yet having taken hold, but one thing I do: forgetting the things which are behind and stretching forward to the things which are before,
Ndugu zangu, sidhani kwamba nimekwisha kupata mambo haya. Bali nafanya jambo moja: nasahau ya nyuma nayatazamia ya mbele.
14 I press on toward the goal for the prize of the high calling of God in Christ Jesus.
Najitahidi kufikia lengo kusudi ili nipate tuzo ya juu ya wito wa Mungu katika Kristo Yesu.
15 Let us therefore, as many as are perfect, think this way. If in anything you think otherwise, God will also reveal that to you.
Sote tulio ukulia wokovu, tunapaswa kuwaza namna hii. Na ikiwa mwingine atafikiri kwa namna iliyotofauti kuhusu jambo lo lote, Mungu pia atalifunuao hiilo kwenu.
16 Nevertheless, to the extent that we have already attained, let’s walk by the same rule. Let’s be of the same mind.
Hata hivyo, hatua ifikia na tuenende katika mtindo huo.
17 Brothers, be imitators together of me, and note those who walk this way, even as you have us for an example.
Ndugu zangu, niigeni mimi. Waangalieni kwa makini wale wanaoenenda kwa mfano ulio wa jinsi yetu.
18 For many walk, of whom I told you often, and now tell you even weeping, as the enemies of the cross of Christ,
Wengi wanaoishi niwale ambao mara nyingi nimewaambieni, na sasa nawaambia kwa machozi -wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.
19 whose end is destruction, whose god is the belly, and whose glory is in their shame, who think about earthly things.
Mwisho wao ni uharibifu. Kwa kuwa Mungu wao ni tumbo, na kiburi chao kiko katika aibu yao. Wanafikiria mambo ya kidunia.
20 For our citizenship is in heaven, from where we also wait for a Savior, the Lord Jesus Christ,
Bali uraia wetu uko mbinguni, ambako tunamtarajia mwokozi wetu Yesu Kristo.
21 who will change the body of our humiliation to be conformed to the body of his glory, according to the working by which he is able even to subject all things to himself.
Atabadilisha miili yetu dhaifu kuwa kama mwili wake wa utukufu; kwa uweza ule ule unaomwezesha kuvidhibiti vitu vyote.

< Philippians 3 >