< Philippians 2 >

1 If therefore there is any exhortation in Christ, if any consolation of love, if any fellowship of the Spirit, if any tender mercies and compassion,
Ikiwa kuna kutiwa moyo katika Kristo. Ikiwa kuna faraja kutoka katika pendo lake. Ikiwa kuna ushirika wa Roho. Ikiwa kuna rehema na huruma.
2 make my joy full by being like-minded, having the same love, being of one accord, of one mind;
Ikamilisheni furaha yangu kwa kunia mamoja mkiwa na upendo mmoja, mkiwa wamoja katika roho, na kuwa na kusudi moja.
3 doing nothing through rivalry or through conceit, but in humility, each counting others better than himself;
Msifanye kwa ubinafsi na majivuno. Isipokuwa kwa unyenyekevu mkiwaona wengine kuwa bora zaidi yenu.
4 each of you not just looking to his own things, but each of you also to the things of others.
Kila mmoja wenu asiangalie tu mahitaji yake binafsi, bali pia ajali mahitaji ya wengine.
5 Have this in your mind, which was also in Christ Jesus,
Muwe na nia kama aliyonayo Kristo Yesu.
6 who, existing in the form of God, didn’t consider equality with God a thing to be grasped,
Ingawaje yeye ni sawa na Mungu. Lakini hakujali kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho.
7 but emptied himself, taking the form of a servant, being made in the likeness of men.
Badala yake, alijishusha mwenyewe. Alichukua umbo la mtumishi. Akajitokeza katika mfano wa wanadamu. Alionekana mwanadamu.
8 And being found in human form, he humbled himself, becoming obedient to the point of death, yes, the death of the cross.
Yeye alijinyeyekeza na kuwa mtii hadi kifo, kifo cha msalaba.
9 Therefore God also highly exalted him, and gave to him the name which is above every name,
Hivyo basi Mungu alimtukuza sana. Alimpa jina kuu lipitalo kila jina.
10 that at the name of Jesus every knee should bow, of those in heaven, those on earth, and those under the earth,
Alifanya hivyo ili kwamba katika jina la Yesu kila goti sharti liiname. Magoti ya walio mbinguni na walio juu ya ardhi na chini ya ardhi.
11 and that every tongue should confess that Jesus Christ is Lord, to the glory of God the Father.
Na alifanya hivyo ili kwamba kila ulimi sharti ukiri kwamba Yesu kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
12 So then, my beloved, even as you have always obeyed, not only in my presence, but now much more in my absence, work out your own salvation with fear and trembling.
Kwa hiyo basi, wapendwa wangu kama mnavyotii siku zote, Si tu katika uwepo wangu lakini sasa ni zaidi sana hata pasipo uwepo wangu, uwajibikeni wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka.
13 For it is God who works in you both to will and to work for his good pleasure.
Kwa kuwa ni Mungu anayetenda kazi ndani yenu ili kuwawezesha kunia na kutenda mambo yale yampendezayo yeye.
14 Do all things without complaining and arguing,
Fanyeni mambo yote bila malalamiko na mabishano.
15 that you may become blameless and harmless, children of God without defect in the middle of a crooked and perverse generation, among whom you are seen as lights in the world,
Fanyeni hivyo ili kwamba msilaumike na kuwa watoto wa Mungu waaminifu wasiyo na lawama. Fanyeni hivyo ili kwamba muwe nuru ya dunia, katika kizazi cha uasi na uovu.
16 holding up the word of life, that I may have something to boast in the day of Christ that I didn’t run in vain nor labor in vain.
Shikani sana neno la uzima ili kwamba niwe na sababu ya kutukuza siku ya Kristo. Kisha nitafahamu kwamba sikupiga mbio bure wala sikutaabika bure.
17 Yes, and if I am poured out on the sacrifice and service of your faith, I am glad and rejoice with you all.
Lakini hata kama ninamiminwa kama sadaka juu ya dhabidhu na huduma ya imani yenu, ninafurahi, na ninafurahi pamoja nanyi nyote.
18 In the same way, you also should be glad and rejoice with me.
Vilevile na ninyi pia mnafurahi, na mnafurahi pamoja nami.
19 But I hope in the Lord Jesus to send Timothy to you soon, that I also may be cheered up when I know how you are doing.
Lakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili kwamba niweze kutiwa moyo nitakapojua mambo yenu.
20 For I have no one else like-minded, who will truly care about you.
Kwa kuwa sina mwingine aliye na mtazamo kama wake, mwenye nia ya kweli kwa ajili yenu.
21 For they all seek their own, not the things of Jesus Christ.
Wengine wote ambao ningewatuma kwenu wanatafuta mambo yao binafsi tu, na siyo mambo ya Yesu Kristo.
22 But you know that he has proved himself. As a child serves a father, so he served with me in furtherance of the Good News.
Lakini mnaijua thamani yake, kwa sababu kama mtoto anavyomhudumia baba yake, ndivyo alivyotumika pamoja nami katika injili.
23 Therefore I hope to send him at once, as soon as I see how it will go with me.
Kwa hiyo ninatumaini kumtuma haraka pindi tu nitakapofahamu nini kitatokea kwangu.
24 But I trust in the Lord that I myself also will come shortly.
Lakini nina hakika katika Bwana kwamba mimi mwenyewe pia nitakuja hivi karibuni.
25 But I thought it necessary to send to you Epaphroditus, my brother, fellow worker, fellow soldier, and your apostle and servant of my need,
Lakini nafikiri ni muhimu kumrejesha kwenu Epafradito. Yeye ni ndugu yangu na mtenda kazi mwenzangu na askari mwenzangu, mjumbe na mtumishi wenu kwa ajili ya mahitaji yangu.
26 since he longed for you all, and was very troubled because you had heard that he was sick.
Kwa sababu alikuwa na hofu na alitamani kuwa pamoja nanyi nyote, kwa kuwa mlisikia kwamba alikuwa mgonjwa.
27 For indeed he was sick nearly to death, but God had mercy on him, and not on him only, but on me also, that I might not have sorrow on sorrow.
Maana hakika alikuwa mgonjwa sana kiasi cha kufa. Lakini Mungu alimhurumia, na wema huo haukuwa juu yake tu, lakini pia ulikuwa juu yangu, ili kwamba nisiwe na huzuni juu ya huzuni.
28 I have sent him therefore the more diligently, that when you see him again, you may rejoice, and that I may be the less sorrowful.
Kwa hiyo ninamrejesha kweny haraka iwezekanavyo, Ili kwamba mtakapomwona tena mpate kufurahi na mimi nitakuwa nimeondolewa wasi wasi.
29 Receive him therefore in the Lord with all joy, and hold such people in honor,
Mkaribisheni Epafradito katika Bwana kwa furaha zote. Waheshimuni watu kama yeye.
30 because for the work of Christ he came near to death, risking his life to supply that which was lacking in your service toward me.
Kwa kuwa ilikuwa kwa ajili ya kazi ya Kristo kwamba alikaribia kufa. Alihatarisha maisha yake ili kuniokoa mimi na akafanya kile ambacho hamkuweza kufanya katika kunihudumia mimi kwa mko mbali nami.

< Philippians 2 >