< Matthew 11 >

1 When Jesus had finished directing his twelve disciples, he departed from there to teach and preach in their cities.
Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka plae kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao,
2 Now when John heard in the prison the works of Christ, he sent two of his disciples
na Yohana akiwa gereszani aliposikia akiwa juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake,
3 and said to him, “Are you he who comes, or should we look for another?”
na wakamuuliza, “Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?”
4 Jesus answered them, “Go and tell John the things which you hear and see:
Yesu akajibu na kusema kwao “Nendeni mkamtaarifu Yohana yale mnayoyaona na yale mnayoyasikia.
5 the blind receive their sight, the lame walk, the lepers are cleansed, the deaf hear, the dead are raised up, and the poor have good news preached to them.
Watu wasioona wanapata kuona, viwete wanatembea, wakoma wanatakaswa, watu wasiosikia wanasikia tena, watu waliokufa wanafufuliwa kupata uhai, na watu wahitaji wanahubiriwa habari njema.
6 Blessed is he who finds no occasion for stumbling in me.”
Na amebarikiwa yule asiyeona shaka juu yangu.
7 As these went their way, Jesus began to say to the multitudes concerning John, “What did you go out into the wilderness to see? A reed shaken by the wind?
Pindi watu hawa walipoondoka, Yesu alianza kusema na umati juu ya Yohana, “Ni nini mlikwenda kuona katika jangwa tete likitikiswa na upepo?
8 But what did you go out to see? A man in soft clothing? Behold, those who wear soft clothing are in kings’ houses.
Lakini nini mlikwenda kuona mtu aliyevaa mavazi mololo? Hakika, wale wavaao mavazi mololo hukaa katika nyumba za wafalme.
9 But why did you go out? To see a prophet? Yes, I tell you, and much more than a prophet.
Lakini mliondoka kuona nini-Nabii? Ndiyo, nawaambia, na zaidi ya Nabii.
10 For this is he, of whom it is written, ‘Behold, I send my messenger before your face, who will prepare your way before you.’
Huyu ndiye aliyeandikiwa, 'Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, ambaye ataandaa njia yako mbele yako.
11 Most certainly I tell you, among those who are born of women there has not arisen anyone greater than John the Baptizer; yet he who is least in the Kingdom of Heaven is greater than he.
Mimi nawaambia kweli, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkubwa kuliko yeye.
12 From the days of John the Baptizer until now, the Kingdom of Heaven suffers violence, and the violent take it by force.
Toka siku za Yohana Mbatizaji mpaka sasa, ufalme wa Mbinguni ni wa nguvu, na watu wenye nguvu, huuchukua kwa nguvu.
13 For all the prophets and the law prophesied until John.
Kwa kuwa manabii na sheria, ikamelcuwa wakitabiri mpaka kwa Yohana.
14 If you are willing to receive it, this is Elijah, who is to come.
Na kamamko tayari kukubali, huyu ni Eliya, yule ajaye.
15 He who has ears to hear, let him hear.
Aliye na masikio ya kusikia na asikie.
16 “But to what shall I compare this generation? It is like children sitting in the marketplaces, who call to their companions
Nikilinganishe na nini kizazi hiki? Ni mfano wa watoto wanaocheza maeneo ya sokoni, wanaokaa na kuitana
17 and say, ‘We played the flute for you, and you didn’t dance. We mourned for you, and you didn’t lament.’
na kusema, 'Tuliwapigia zomari na hamkucheza. Tuliomboleza, na hamukulia.'
18 For John came neither eating nor drinking, and they say, ‘He has a demon.’
Kwa kuwa Yohana alikuja bila kula mkate au kunywa mvinyo, na wakawa wanasema, 'Ana pepo.'
19 The Son of Man came eating and drinking, and they say, ‘Behold, a gluttonous man and a drunkard, a friend of tax collectors and sinners!’ But wisdom is justified by her children.”
Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema 'Angalia, ni mtu mlaji na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!' Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.''
20 Then he began to denounce the cities in which most of his mighty works had been done, because they didn’t repent.
Yesu alianza kuikemea miji ambamo baadhi ya matendo yake ya ajabu yalitendeka, kwa sababu walikuwa hawajatubu,
21 “Woe to you, Chorazin! Woe to you, Bethsaida! For if the mighty works had been done in Tyre and Sidon which were done in you, they would have repented long ago in sackcloth and ashes.
Ole wako, Kolazini, Ole wako Bethsaida! Kama matendo makuu yangetendeka Tiro na Sidoni yale yaliyotendeka hapa, wangekuwa wametubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.
22 But I tell you, it will be more tolerable for Tyre and Sidon on the day of judgment than for you.
Lakini itakuwa uvumilivu kwa Tiro na Sidoni siku ya hukumu kuliko kwako.
23 You, Capernaum, who are exalted to heaven, you will go down to Hades. For if the mighty works had been done in Sodom which were done in you, it would have remained until today. (Hadēs g86)
Wewe, Kapernaum, unadhani utainuliwa hadi mbinguni? Hapana utashushwa hadi chini kuzimu. Kama kwa Sodoma kungefanyika matendo makuu, kama yalifanyika kwako, ingekuwepo hadi leo. (Hadēs g86)
24 But I tell you that it will be more tolerable for the land of Sodom on the day of judgment, than for you.”
Bali nasema kwako kwamba itakuwa rahisi kwa nchi ya Sodoma kusimama siku ya hukumu kuliko wewe.
25 At that time, Jesus answered, “I thank you, Father, Lord of heaven and earth, that you hid these things from the wise and understanding, and revealed them to infants.
Katika muda huo Yesu alisema, “Nakusifu wewe, Baba, Bwana wa Mbingu na Nchi, kwa sababu uliwaficha mambo haya wenye hekima na ufahamu, na kuyafunua kwa wasio na elimu, kama watoto wadogo.
26 Yes, Father, for so it was well-pleasing in your sight.
Baba kwa kuwa ilikupendeza hivyo machoni pako.
27 All things have been delivered to me by my Father. No one knows the Son, except the Father; neither does anyone know the Father, except the Son and he to whom the Son desires to reveal him.
Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia.
28 “Come to me, all you who labor and are heavily burdened, and I will give you rest.
Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha.
29 Take my yoke upon you and learn from me, for I am gentle and humble in heart; and you will find rest for your souls.
Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu.
30 For my yoke is easy, and my burden is light.”
Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.

< Matthew 11 >