< Matthew 10 >

1 He called to himself his twelve disciples, and gave them authority over unclean spirits, to cast them out, and to heal every disease and every sickness.
Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.
2 Now the names of the twelve apostles are these. The first, Simon, who is called Peter; Andrew, his brother; James the son of Zebedee; John, his brother;
Majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya: wa kwanza ni Simoni aitwae Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohane ndugu yake;
3 Philip; Bartholomew; Thomas; Matthew the tax collector; James the son of Alphaeus; Lebbaeus, who was also called Thaddaeus;
Filipo na Bartholomayo, Thoma na Mathayo aliyekuwa mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo;
4 Simon the Zealot; and Judas Iscariot, who also betrayed him.
Simoni Mkanaani, na Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.
5 Jesus sent these twelve out and commanded them, saying, “Don’t go among the Gentiles, and don’t enter into any city of the Samaritans.
Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika mji wa Wasamaria.
6 Rather, go to the lost sheep of the house of Israel.
Ila nendeni kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo.
7 As you go, preach, saying, ‘The Kingdom of Heaven is at hand!’
Mnapokwenda hubirini hivi: Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 Heal the sick, cleanse the lepers, and cast out demons. Freely you received, so freely give.
Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo. Mmepewa bure, toeni bure.
9 Don’t take any gold, silver, or brass in your money belts.
Msichukue mifukoni mwenu dhahabu, wala fedha, wala sarafu za shaba.
10 Take no bag for your journey, neither two coats, nor sandals, nor staff: for the laborer is worthy of his food.
Msichukue mkoba wa kuombea njiani, wala koti la ziada, wala viatu, wala fimbo. Maana mfanyakazi anastahili riziki yake.
11 Into whatever city or village you enter, find out who in it is worthy, and stay there until you go on.
“Mkiingia katika mji wowote au kijiji, tafuteni humo mtu yeyote aliye tayari kuwakaribisheni, na kaeni naye mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
12 As you enter into the household, greet it.
Mnapoingia nyumbani wasalimuni wenyeji wake.
13 If the household is worthy, let your peace come on it, but if it isn’t worthy, let your peace return to you.
Kama wenyeji wa nyumba hiyo wakiipokea salamu hiyo, basi, amani yenu itakaa pamoja nao. Lakini ikiwa hawaipokei, basi amani yenu itawarudia ninyi.
14 Whoever doesn’t receive you or hear your words, as you go out of that house or that city, shake the dust off your feet.
Kama mtu yeyote atakataa kuwakaribisheni au kuwasikilizeni, basi mtokapo katika nyumba hiyo au mji huo, yakung'uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.
15 Most certainly I tell you, it will be more tolerable for the land of Sodom and Gomorrah in the day of judgment than for that city.
Kweli nawaambieni, Siku ya hukumu mji huo utapata adhabu kubwa kuliko ile iliyoipata miji ya Sodoma na Gomora.
16 “Behold, I send you out as sheep among wolves. Therefore be wise as serpents and harmless as doves.
“Sasa, mimi nawatuma ninyi kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.
17 But beware of men, for they will deliver you up to councils, and in their synagogues they will scourge you.
Jihadharini na watu, maana watawapeleka ninyi mahakamani na kuwapiga viboko katika masunagogi yao.
18 Yes, and you will be brought before governors and kings for my sake, for a testimony to them and to the nations.
Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, mpate kutangaza Habari Njema kwao na kwa mataifa.
19 But when they deliver you up, don’t be anxious how or what you will say, for it will be given you in that hour what you will say.
Basi, watakapowapeleka ninyi mahakamani, msiwe na wasiwasi mtasema nini au namna gani; wakati utakapofika, mtapewa la kusema.
20 For it is not you who speak, but the Spirit of your Father who speaks in you.
Maana si ninyi mtakaosema, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.
21 “Brother will deliver up brother to death, and the father his child. Children will rise up against parents and cause them to be put to death.
“Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanawe, nao watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
22 You will be hated by all men for my name’s sake, but he who endures to the end will be saved.
Watu wote watawachukieni kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa.
23 But when they persecute you in this city, flee into the next, for most certainly I tell you, you will not have gone through the cities of Israel until the Son of Man has come.
“Watu wakiwadhulumu katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kweli nawaambieni, hamtamaliza ziara yenu katika miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Mtu hajafika.
24 “A disciple is not above his teacher, nor a servant above his lord.
“Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumishi si mkuu kuliko bwana wake.
25 It is enough for the disciple that he be like his teacher, and the servant like his lord. If they have called the master of the house Beelzebul, how much more those of his household!
Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wa jamaa Beelzebuli, je hawatawaita watu wengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?
26 Therefore don’t be afraid of them, for there is nothing covered that will not be revealed, or hidden that will not be known.
“Basi, msiwaogope watu hao. Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, na kila kilichofichwa kitafichuliwa.
27 What I tell you in the darkness, speak in the light; and what you hear whispered in the ear, proclaim on the housetops.
Ninalowaambieni ninyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na jambo mlilosikia likinong'onezwa, litangazeni hadharani.
28 Don’t be afraid of those who kill the body, but are not able to kill the soul. Rather, fear him who is able to destroy both soul and body in Gehenna. (Geenna g1067)
Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa Jehanamu. (Geenna g1067)
29 “Aren’t two sparrows sold for an assarion coin? Not one of them falls to the ground apart from your Father’s will.
Shomoro wawili huuzwa kwa senti tano. Lakini hata mmoja wao haanguki chini bila kibali cha Baba yenu.
30 But the very hairs of your head are all numbered.
Lakini kwa upande wenu, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.
31 Therefore don’t be afraid. You are of more value than many sparrows.
Kwa hiyo msiogope; ninyi mu wa thamani kuliko shomoro wengi.
32 Everyone therefore who confesses me before men, I will also confess him before my Father who is in heaven.
“Kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
33 But whoever denies me before men, I will also deny him before my Father who is in heaven.
Lakini yeyote atakayenikana hadharani, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
34 “Don’t think that I came to send peace on the earth. I didn’t come to send peace, but a sword.
“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.
35 For I came to set a man at odds against his father, and a daughter against her mother, and a daughter-in-law against her mother-in-law.
Maana nimekuja kuleta mafarakano kati ya mtu na baba yake, kati ya binti na mama yake, kati ya mkwe na mkwe wake.
36 A man’s foes will be those of his own household.
Na maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake.
37 He who loves father or mother more than me is not worthy of me; and he who loves son or daughter more than me isn’t worthy of me.
“Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 He who doesn’t take his cross and follow after me isn’t worthy of me.
Mtu asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hanistahili.
39 He who seeks his life will lose it; and he who loses his life for my sake will find it.
Anayeyashikilia maisha yake, atayapoteza; lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata.
40 “He who receives you receives me, and he who receives me receives him who sent me.
“Anayewakaribisha ninyi, ananikaribisha mimi; na anayenikaribisha mimi, anamkaribisha yule aliyenituma.
41 He who receives a prophet in the name of a prophet will receive a prophet’s reward. He who receives a righteous man in the name of a righteous man will receive a righteous man’s reward.
Anayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii, atapokea tuzo la nabii. Anayemkaribisha mtu mwema kwa sababu ni mtu mwema, atapokea tuzo la mtu mwema.
42 Whoever gives one of these little ones just a cup of cold water to drink in the name of a disciple, most certainly I tell you, he will in no way lose his reward.”
Kweli nawaambieni, yeyote atakayempa mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji baridi kwa sababu ni mfuasi wangu, hatakosa kamwe kupata tuzo lake.”

< Matthew 10 >