< John 18 >

1 When Jesus had spoken these words, he went out with his disciples over the brook Kidron, where there was a garden, into which he and his disciples entered.
Baada ya Yesu kusema maneno haya, aliondoka na wanafunzi wake kuelekea bonde la Kidron, ambako kulikuwa na bustani, ambako yeye na wanafunzi wake wakaingia ndani yake.
2 Now Judas, who betrayed him, also knew the place, for Jesus often met there with his disciples.
Sasa yule Yuda, aliyetaka kumsaliti, naye alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akienda hili eneo mara kadhaa akiwa na wanafunzi wake.
3 Judas then, having taken a detachment of soldiers and officers from the chief priests and the Pharisees, came there with lanterns, torches, and weapons.
Naye Yuda, baada ya kuwa amepata kundi la maaskari na maofisa toka kwa wakuu wa makuhani, wakaja wakiwa na taa, kurunzi na silaha.
4 Jesus therefore, knowing all the things that were happening to him, went out and said to them, “Who are you looking for?”
Naye Yesu, hali akijua kila kitu kilichokuwa kikifanyika dhidi yake, alijitokeza mbele na akawauliza, “Ni nani mnayemtafuta?”
5 They answered him, “Jesus of Nazareth.” Jesus said to them, “I am he.” Judas also, who betrayed him, was standing with them.
Nao wakamjibu, “Yesu Mnazareth.” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye” Naye Yuda aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja na wale askari.
6 When therefore he said to them, “I am he,” they went backward and fell to the ground.
Kwa hiyo alipowaambia, “Mimi ndiye” walirudi kinyume na kuanguka chini.
7 Again therefore he asked them, “Who are you looking for?” They said, “Jesus of Nazareth.”
Halafu akawauliza tena, “Ni nani mnayemtafuta? Nao wakamjibu tena “Yesu mnazareth.”
8 Jesus answered, “I told you that I am he. If therefore you seek me, let these go their way,”
Yesu akawajibu, “Nimekwisha kuwaambia kuwa Mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa wengine waende.”
9 that the word might be fulfilled which he spoke, “Of those whom you have given me, I have lost none.”
Haya yalikuwa hivyo ili lile neno litimilike; pale aliposema; “Katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmoja.”
10 Simon Peter therefore, having a sword, drew it, struck the high priest’s servant, and cut off his right ear. The servant’s name was Malchus.
Ndipo Simon Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani mkuu. Na jina lake mtumishi yule lilikuwa Malko.
11 Jesus therefore said to Peter, “Put the sword into its sheath. The cup which the Father has given me, shall I not surely drink it?”
Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Kwa nini nisikinywee kikombe kile alichonipa Baba?”
12 So the detachment, the commanding officer, and the officers of the Jews seized Jesus and bound him,
Basi lile kundi la askari na jemedari, na watumishi wa Wayahudi, walimkamata Yesu na kumfunga.
13 and led him to Annas first, for he was father-in-law to Caiaphas, who was high priest that year.
Nao wakamwongoza kwanza mpaka kwa Anasi, kwani yeye alikuwa mkwe wa Kayafa, ambaye ndiye aliyekuwa Kuhani mkuu kwa mwaka huo.
14 Now it was Caiaphas who advised the Jews that it was expedient that one man should perish for the people.
Sasa Kayafa ndiye aliyekuwa amewapa ushauri Wayahudi ya kwamba ilimpasa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
15 Simon Peter followed Jesus, as did another disciple. Now that disciple was known to the high priest, and entered in with Jesus into the court of the high priest;
Simon Petro alimfuata Yesu, na vivyo hivyo mwanafunzi mwingine. Na yule mwanafunzi alikuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, naye akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani mkuu;
16 but Peter was standing at the door outside. So the other disciple, who was known to the high priest, went out and spoke to her who kept the door, and brought in Peter.
lakini Petro alikuwa amesimama nje ya mlango. Basi yule mwanafunzi aliyekuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, alitoka nje akaenda kuongea na yule mwanamke mtumishi aliyekuwa akilinda mlango na kumwingiza Petro ndani.
17 Then the maid who kept the door said to Peter, “Are you also one of this man’s disciples?” He said, “I am not.”
Basi yule kijakazi aliyekuwa akilinda mlango, alimwambia Petro, “Je wewe si mmoja wa wafuasi wa huyu mtu?” Naye akasema, “Mimi siye.”
18 Now the servants and the officers were standing there, having made a fire of coals, for it was cold. They were warming themselves. Peter was with them, standing and warming himself.
Na wale watumishi na wakuu walikuwa wakisimama mahali pale; wamekoka moto wa kwa maana, kulikuwa na baridi, na hivyo walikuwa wakiota moto ili kupata joto. Naye Petro alikuwa nao, akiota moto akiwa amesimama.
19 The high priest therefore asked Jesus about his disciples and about his teaching.
Kuhani mkuu alimhoji Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake.
20 Jesus answered him, “I spoke openly to the world. I always taught in synagogues and in the temple, where the Jews always meet. I said nothing in secret.
Yesu akamjbu, “Nimeuambia waziwazi ulimwengu; Mimi nilifundisha mara kwa mara kwenye masinagogi na hekaluni mahali ambapo wayahudi hukusanyika. Nami sikusema lolote katika siri.
21 Why do you ask me? Ask those who have heard me what I said to them. Behold, they know the things which I said.”
Kwa nini mliniuliza? Waulizeni walionisikiliza juu ya kile nilichosema. Hawa watu wanajua mambo yale niliyosema.
22 When he had said this, one of the officers standing by slapped Jesus with his hand, saying, “Do you answer the high priest like that?”
Yesu alipokwisha sema hivyo, mmoja wa wakuu aliyekuwa amesimama akampiga Yesu kwa mkono wake na kisha akasema, “Je, hivyo ndivyo inavyokupasa kumjibu kuhani mkuu?”
23 Jesus answered him, “If I have spoken evil, testify of the evil; but if well, why do you beat me?”
Naye Yesu akamjibu, “Kama nimesema jambo lolote baya basi uwe shahidi kwa ajili ya uovu, na kama nimemjibu vyema kwa nini kunipiga?
24 Annas sent him bound to Caiaphas, the high priest.
Ndipo Anasi alipompeleka Yesu kwa Kayafa kuhani mkuu akiwa amefungwa.
25 Now Simon Peter was standing and warming himself. They said therefore to him, “You aren’t also one of his disciples, are you?” He denied it and said, “I am not.”
Sasa Simoni Petro alikuwa amesimama akijipasha joto mwenyewe. Halafu wale watu wakamwambia. “Je, wewe pia si mmoja wa wanaafunzi wake?” Akakana akisema “Mimi siye.”
26 One of the servants of the high priest, being a relative of him whose ear Peter had cut off, said, “Didn’t I see you in the garden with him?”
Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ambaye alikuwa ndugu wa yule mwanaume ambaye Petro alimkata sikio, alisema, “Je si wewe niliyekuona naye kule bustanini?”
27 Peter therefore denied it again, and immediately the rooster crowed.
Petro akakana tena, na mara Jogoo akawika.
28 They led Jesus therefore from Caiaphas into the Praetorium. It was early, and they themselves didn’t enter into the Praetorium, that they might not be defiled, but might eat the Passover.
Kisha wakamchukua Yesu toka kwa Kayafa mpaka kwenye Praitorio. Ilikwa asubuhi na mapema. Wao wenyewe hawakuiingia ile Praitorio ili wasije wakanajisika na kuila pasaka.
29 Pilate therefore went out to them and said, “What accusation do you bring against this man?”
Kwa hiyo Pilato akawaendea akisema. “Ni shitaka gani linalomhusu huyu mtu?”
30 They answered him, “If this man weren’t an evildoer, we wouldn’t have delivered him up to you.”
Wakamjibu na kumwambia, “Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako.”
31 Pilate therefore said to them, “Take him yourselves, and judge him according to your law.” Therefore the Jews said to him, “It is illegal for us to put anyone to death,”
Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kulingana na sheria yenu.” Nao Wayahudi wakamwambia, “Sheria haituruhusu sisi kumwua mtu yeyote.”
32 that the word of Jesus might be fulfilled, which he spoke, signifying by what kind of death he should die.
Walisema haya ili neno la Yesu litimilike, neno ambalo alikuwa amekwisha sema juu ya aina ya kifo chake.
33 Pilate therefore entered again into the Praetorium, called Jesus, and said to him, “Are you the King of the Jews?”
Basi Pilato akaingia tena Praitorio akumwita Yesu; akamwambia, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?”
34 Jesus answered him, “Do you say this by yourself, or did others tell you about me?”
Yesu akamjibu, “Je, wewe waniuliza swali hili kwa Sababu wataka kujua au kwa sababu wengine wamekutuma ili uniulize mimi?”
35 Pilate answered, “I’m not a Jew, am I? Your own nation and the chief priests delivered you to me. What have you done?”
Naye Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, au sivyo?” Taifa lako na kuhani mkuu ndio waliokuleta kwangu; wewe umefanya nini?
36 Jesus answered, “My Kingdom is not of this world. If my Kingdom were of this world, then my servants would fight, that I wouldn’t be delivered to the Jews. But now my Kingdom is not from here.”
Yesu akajibu; “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa na sehemu katika ulimwengu huu watumwa wangu wangenipigania ili nisitolewe kwa wayahudi. Kwa kweli ufalme wangu hautoki hapa” Basi
37 Pilate therefore said to him, “Are you a king then?” Jesus answered, “You say that I am a king. For this reason I have been born, and for this reason I have come into the world, that I should testify to the truth. Everyone who is of the truth listens to my voice.”
Pilato akamwambia, “Je, wewe basi u mfalme?” Yesu akajibu, “wewe ndivyo unanvyosema kuwa mimi ni mfalme, Kwa sababu hii mimi nilizaliwa na kwa sababu hii mimi nimekuja ulimwenguni ili niwe shahidi wa ile kweli. Yeyote aliye wa hiyo kweli huisikiliza sauti yangu.
38 Pilate said to him, “What is truth?” When he had said this, he went out again to the Jews, and said to them, “I find no basis for a charge against him.
Pilato akamwambia, “Kweli ni nini?” Naye alipokwisha sema haya akaenda kwa Wayahudi na kuwaambia “Siona katika lolote mtu huyu.
39 But you have a custom that I should release someone to you at the Passover. Therefore, do you want me to release to you the King of the Jews?”
Ninyi mna utamaduni unaonifanya nimfunfungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Je mnataka nimfungulie mfalme wa Wayahudi.”
40 Then they all shouted again, saying, “Not this man, but Barabbas!” Now Barabbas was a robber.
Kisha walipiga kelele wakisema, siyo huyu, tufungulie Baraba.” Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.

< John 18 >