< Ezekiel 29 >

1 In the tenth year, in the tenth month, on the twelfth day of the month, Yahweh’s word came to me, saying,
Katika mwaka wa kumi, mwezi wa kumi, siku ya kumi na mbili, neno la Bwana likanijia kusema:
2 “Son of man, set your face against Pharaoh king of Egypt, and prophesy against him and against all Egypt.
“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Farao mfalme wa Misri na utabiri dhidi yake na dhidi ya Misri yote.
3 Speak and say, ‘The Lord Yahweh says: “Behold, I am against you, Pharaoh king of Egypt, the great monster that lies in the middle of his rivers, that has said, ‘My river is my own, and I have made it for myself.’
Nena, nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Mimi ni kinyume nawe, Farao, mfalme wa Misri, joka kubwa ulalaye katikati ya vijito vyako. Unasema, “Mto Naili ni wangu mwenyewe; niliufanya kwa ajili yangu mwenyewe.”
4 I will put hooks in your jaws, and I will make the fish of your rivers stick to your scales. I will bring you up out of the middle of your rivers, with all the fish of your rivers which stick to your scales.
Lakini nitatia ndoana katika mataya yako nami nitawafanya samaki wa vijito vyako washikamane na magamba yako. Nitakutoa katikati ya vijito vyako, pamoja na samaki wote walioshikamana na magamba yako.
5 I’ll cast you out into the wilderness, you and all the fish of your rivers. You’ll fall on the open field. You won’t be brought together or gathered. I have given you for food to the animals of the earth and to the birds of the sky.
Nitakutupa jangwani, wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako. Utaanguka uwanjani, nawe hutakusanywa au kuchukuliwa. Nitakutoa uwe chakula kwa wanyama wa nchi na ndege wa angani.
6 “‘“All the inhabitants of Egypt will know that I am Yahweh, because they have been a staff of reed to the house of Israel.
Ndipo wale wote waishio Misri watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana. “‘Umekuwa fimbo ya tete kwa nyumba ya Israeli.
7 When they took hold of you by your hand, you broke and tore all their shoulders. When they leaned on you, you broke and paralyzed all of their thighs.”
Walipokushika kwa mikono yao, ulivunjika na kuchana mabega yao; walipokuegemea, ulivunjika na migongo yao ikateguka.
8 “‘Therefore the Lord Yahweh says: “Behold, I will bring a sword on you, and will cut off man and animal from you.
“‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaleta upanga juu yako na kuua watu wako na wanyama wao.
9 The land of Egypt will be a desolation and a waste. Then they will know that I am Yahweh. “‘“Because he has said, ‘The river is mine, and I have made it,’
Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana. “‘Kwa sababu ulisema, “Mto Naili ni wangu; mimi niliufanya,”
10 therefore, behold, I am against you and against your rivers. I will make the land of Egypt an utter waste and desolation, from the tower of Seveneh even to the border of Ethiopia.
kwa hiyo mimi ni kinyume nawe na kinyume na vijito vyako, nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa magofu na ukiwa isiyolimwa wala kukaliwa na watu kuanzia Migdoli hadi Aswani, hata kufikia mpakani wa Ethiopia.
11 No foot of man will pass through it, nor will any animal foot pass through it. It won’t be inhabited for forty years.
Hakuna unyayo wa mtu au mnyama utakaopita ndani yake, wala hakuna yeyote atakayeishi humo kwa muda wa miaka arobaini.
12 I will make the land of Egypt a desolation in the middle of the countries that are desolate. Her cities among the cities that are laid waste will be a desolation forty years. I will scatter the Egyptians among the nations, and will disperse them through the countries.”
Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi nyingine.
13 “‘For the Lord Yahweh says: “At the end of forty years I will gather the Egyptians from the peoples where they were scattered.
“‘Lakini hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mwishoni mwa hiyo miaka arobaini, nitawakusanya Wamisri kutoka mataifa walikotawanywa.
14 I will reverse the captivity of Egypt, and will cause them to return into the land of Pathros, into the land of their birth. There they will be a lowly kingdom.
Nitawarudisha hao Wamisri kutoka kwenye kutekwa kwao na kuwaweka katika Pathrosi, nchi ya baba zao. Huko watakuwa na ufalme usiokuwa na nguvu.
15 It will be the lowest of the kingdoms. It won’t lift itself up above the nations any more. I will diminish them so that they will no longer rule over the nations.
Utakuwa ufalme dhaifu kuliko zote na kamwe Misri haitajikweza tena juu ya mataifa mengine. Nitaufanya ufalme wake dhaifu sana kiasi kwamba kamwe hautatawala tena juu ya mataifa mengine.
16 It will no longer be the confidence of the house of Israel, bringing iniquity to memory, when they turn to look after them. Then they will know that I am the Lord Yahweh.”’”
Misri haitakuwa tena tumaini la watu wa Israeli bali itakuwa kumbukumbu ya dhambi yao kwa kuigeukia kuomba msaada. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.’”
17 It came to pass in the twenty-seventh year, in the first month, in the first day of the month, Yahweh’s word came to me, saying,
Katika mwaka wa ishirini na saba, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza, neno la Bwana likanijia, kusema:
18 “Son of man, Nebuchadnezzar king of Babylon caused his army to serve a great service against Tyre. Every head was made bald, and every shoulder was worn; yet he had no wages, nor did his army, from Tyre, for the service that he had served against it.
“Mwanadamu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliongoza jeshi lake kufanya kazi ngumu dhidi ya Tiro; kila kichwa kilipata upaa na kila bega likachunika. Lakini yeye na jeshi lake hawakupata malipo yoyote kutokana na muda wote aliongoza hiyo vita dhidi ya Tiro.
19 Therefore the Lord Yahweh says: ‘Behold, I will give the land of Egypt to Nebuchadnezzar king of Babylon. He will carry off her multitude, take her plunder, and take her prey. That will be the wages for his army.
Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaitia Misri mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye atachukua utajiri wa Misri. Atateka mateka na kuchukua nyara mali za Misri kama ujira kwa ajili ya jeshi lake.
20 I have given him the land of Egypt as his payment for which he served, because they worked for me,’ says the Lord Yahweh.
Nimempa mfalme wa Babeli nchi ya Misri kuwa ujira kwa juhudi zake kwa sababu yeye na jeshi lake walifanya kwa ajili yangu, asema Bwana Mwenyezi.
21 “In that day I will cause a horn to sprout for the house of Israel, and I will open your mouth among them. Then they will know that I am Yahweh.”
“Katika siku hiyo nitaifanya nyumba ya Israeli iwe na nguvu nami nitakifungua kinywa chako miongoni mwao. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.”

< Ezekiel 29 >