< 1 John 1 >

1 That which was from the beginning, that which we have heard, that which we have seen with our eyes, that which we saw, and our hands touched, concerning the Word of life
Kile kilichokuwapo tangu mwanzo-kile tulichokisikia, kile tulichokiona kwa macho yetu, kile tulichokitazama, na mikono yetu imekishika-kuhusu Neno la uzima.
2 (and the life was revealed, and we have seen, and testify, and declare to you the life, the eternal life, which was with the Father, and was revealed to us); (aiōnios g166)
Na ule uzima ulifanywa kujulikana wazi, na tumeuona, na kuushuhudia, na kuwatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa kwa Baba na ulifanywa kujulikana kwetu. (aiōnios g166)
3 that which we have seen and heard we declare to you, that you also may have fellowship with us. Yes, and our fellowship is with the Father and with his Son, Jesus Christ.
Kile tulichokiona na kukisikia twakitangaza kwenu pia, ili kwamba muweze kujumuika pamoja nasi, na ushirika wetu pamoja na Baba na Mwanae Yesu Kristo.
4 And we write these things to you, that our joy may be fulfilled.
Na tunawandikia mambo haya ninyi ili kwamba furaha yetu iwe timilifu.
5 This is the message which we have heard from him and announce to you, that God is light, and in him is no darkness at all.
Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake na kuwatangazia: Mungu ni nuru na ndani yake hakuna giza hata kidogo.
6 If we say that we have fellowship with him and walk in the darkness, we lie and don’t tell the truth.
Kama tukisema kwamba tunaushirika naye na twatembea gizani, twadanganya na hatutendi kweli.
7 But if we walk in the light as he is in the light, we have fellowship with one another, and the blood of Jesus Christ his Son, cleanses us from all sin.
Lakini tukitembea katika nuru kama alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu ya Yesu Kristo, mwanae yatutakasa kutoka dhambi zote.
8 If we say that we have no sin, we deceive ourselves, and the truth is not in us.
Kama tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, na kweli haimo ndani yetu.
9 If we confess our sins, he is faithful and righteous to forgive us the sins and to cleanse us from all unrighteousness.
Lakini tukizitubu dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
10 If we say that we haven’t sinned, we make him a liar, and his word is not in us.
Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, twamfanya yeye kuwa muongo, na neno lake halimo ndani yetu.

< 1 John 1 >