< John 12 >

1 Then, six days before the Passover, Jesus came to Bethany, where Lazarus was, who had been dead, whom he raised from the dead.
Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alifika Bethania alikoishi Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua kutoka wafu.
2 So they made him a supper there. Martha served, but Lazarus was one of those who sat at the table with him.
Huko walimwandalia chakula cha jioni, naye Martha akawa anawatumikia. Lazaro alikuwa mmoja wa wale waliokuwa mezani pamoja na Yesu.
3 Therefore Mary took a pound of ointment of pure nard, very precious, and anointed Jesus’ feet and wiped his feet with her hair. The house was filled with the fragrance of the ointment.
Basi, Maria alichukua chupa ya marashi ya nardo safi ya thamani kubwa, akampaka Yesu miguu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba yote ikajaa harufu ya marashi.
4 Then Judas Iscariot, Simon’s son, one of his disciples, who would betray him, said,
Basi, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,
5 “Why wasn’t this ointment sold for three hundred denarii and given to the poor?”
“Kwa nini marashi hayo hayakuuzwa kwa fedha dinari mia tatu, wakapewa maskini?”
6 Now he said this, not because he cared for the poor, but because he was a thief, and having the money box, used to steal what was put into it.
Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina.
7 But Jesus said, “Leave her alone. She has kept this for the day of my burial.
Lakini Yesu akasema, “Msimsumbue huyu mama! Mwacheni ayaweke kwa ajili ya siku ya mazishi yangu.
8 For you always have the poor with you, but you don’t always have me.”
Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa nami siku zote.”
9 A large crowd therefore of the Jews learned that he was there; and they came, not for Jesus’ sake only, but that they might see Lazarus also, whom he had raised from the dead.
Wayahudi wengi walisikia kwamba Yesu alikuwa Bethania. Basi, wakafika huko si tu kwa ajili ya kumwona Yesu, ila pia wapate kumwona Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka wafu.
10 But the chief priests conspired to put Lazarus to death also,
Makuhani wakuu waliamua pia kumwua Lazaro,
11 because on account of him many of the Jews went away and believed in Jesus.
Maana kwa sababu ya Lazaro Wayahudi wengi waliwaasi viongozi wao, wakamwamini Yesu.
12 On the next day a great multitude had come to the feast. When they heard that Jesus was coming to Jerusalem,
Kesho yake, kundi kubwa la watu waliokuja kwenye sikukuu walisikia kuwa Yesu alikuwa njiani kuja Yerusalemu.
13 they took the branches of the palm trees and went out to meet him, and cried out, “Hosanna! Blessed is he who comes in the name of the Lord, the King of Israel!”
Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaaza sauti wakisema: “Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli.”
14 Jesus, having found a young donkey, sat on it. As it is written,
Yesu akampata mwana punda mmoja akapanda juu yake kama yasemavyo Maandiko:
15 “Don’t be afraid, daughter of Zion. Behold, your King comes, sitting on a donkey’s colt.”
“Usiogope mji wa Sioni! Tazama, Mfalme wako anakuja, Amepanda mwana punda.”
16 His disciples didn’t understand these things at first, but when Jesus was glorified, then they remembered that these things were written about him, and that they had done these things to him.
Wakati huo wanafunzi wake hawakuelewa mambo hayo, lakini Yesu alipokwisha tukuzwa, ndipo walipokumbuka kwamba hayo yalikuwa yameandikwa juu yake, na kwamba watu walikuwa wamemtendea hivyo.
17 The multitude therefore that was with him when he called Lazarus out of the tomb and raised him from the dead was testifying about it.
Kundi la watu wale waliokuwa pamoja naye wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua kutoka wafu, walisema yaliyotukia.
18 For this cause also the multitude went and met him, because they heard that he had done this sign.
Kwa hiyo umati huo wa watu ulimlaki, maana wote walisikia kwamba Yesu alikuwa amefanya ishara hiyo.
19 The Pharisees therefore said among themselves, “See how you accomplish nothing. Behold, the world has gone after him.”
Basi, Mafarisayo wakaambiana, “Mnaona? Hatuwezi kufanya chochote! Tazameni, ulimwengu wote unamfuata.”
20 Now there were certain Greeks among those who went up to worship at the feast.
Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu hiyo.
21 Therefore, these came to Philip, who was from Bethsaida of Galilee, and asked him, saying, “Sir, we want to see Jesus.”
Hao walimwendea Filipo, mwenyeji wa Bethsaida katika Galilaya, wakasema, “Mheshimiwa, tunataka kumwona Yesu.”
22 Philip came and told Andrew, and in turn, Andrew came with Philip, and they told Jesus.
Filipo akaenda akamwambia Andrea, nao wawili wakaenda kumwambia Yesu.
23 Jesus answered them, “The time has come for the Son of Man to be glorified.
Yesu akawaambia, “Saa ya kutukuzwa kwa Mwana wa Mtu imefika!
24 Most certainly I tell you, unless a grain of wheat falls into the earth and dies, it remains by itself alone. But if it dies, it bears much fruit.
Kweli nawaambieni, punje ya ngano hubaki punje tu isipokuwa ikianguka katika udongo na kufa. Kama ikifa, basi huzaa matunda mengi.
25 He who loves his life will lose it. He who hates his life in this world will keep it to eternal life. (aiōnios g166)
Anayependa maisha yake, atayapoteza; anayeyachukia maisha yake katika ulimwengu huu, atayaweka kwa ajili ya uzima wa milele. (aiōnios g166)
26 If anyone serves me, let him follow me. Where I am, there my servant will also be. If anyone serves me, the Father will honor him.
Anayetaka kunitumikia ni lazima anifuate, hivyo kwamba popote pale nilipo mimi ndipo na mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu yeyote anayenitumikia Baba yangu atampa heshima.
27 “Now my soul is troubled. What shall I say? ‘Father, save me from this time’? But I came to this time for this cause.
“Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: Baba, usiruhusu saa hii inifikie? Lakini ndiyo maana nimekuja—ili nipite katika saa hii.
28 Father, glorify your name!” Then a voice came out of the sky, saying, “I have both glorified it and will glorify it again.”
Baba, ulitukuze jina lako.” Hapo sauti ikasema kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, na nitalitukuza tena.”
29 Therefore the multitude who stood by and heard it said that it had thundered. Others said, “An angel has spoken to him.”
Umati wa watu waliokuwa wamesimama hapo walisikia sauti hiyo, na baadhi yao walisema, “Malaika ameongea naye!”
30 Jesus answered, “This voice hasn’t come for my sake, but for your sakes.
Lakini Yesu akawaambia, “Sauti hiyo haikutokea kwa ajili yangu mimi, ila kwa ajili yenu.
31 Now is the judgment of this world. Now the prince of this world will be cast out.
Sasa ndio wakati wa ulimwengu huu kuhukumiwa; sasa mtawala wa ulimwengu huu atapinduliwa.
32 And I, if I am lifted up from the earth, will draw all people to myself.”
Nami nitakapoinuliwa juu ya nchi nitamvuta kila mmoja kwangu.”
33 But he said this, signifying by what kind of death he should die.
(Kwa kusema hivyo alionyesha atakufa kifo gani).
34 The multitude answered him, “We have heard out of the law that the Christ remains forever. How do you say, ‘The Son of Man must be lifted up’? Who is this Son of Man?” (aiōn g165)
Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na Sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?” (aiōn g165)
35 Jesus therefore said to them, “Yet a little while the light is with you. Walk while you have the light, that darkness doesn’t overtake you. He who walks in the darkness doesn’t know where he is going.
Yesu akawaambia, “Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.
36 While you have the light, believe in the light, that you may become children of light.” Jesus said these things, and he departed and hid himself from them.
Basi, wakati mnao huo mwanga uaminini ili mpate kuwa watu wa mwanga.” Baada ya kusema maneno hayo, Yesu alikwenda zake na kujificha mbali nao.
37 But though he had done so many signs before them, yet they didn’t believe in him,
Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbele yao, wao hawakumwamini.
38 that the word of Isaiah the prophet might be fulfilled, which he spoke: “Lord, who has believed our report? To whom has the arm of the Lord been revealed?”
Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia: “Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?”
39 For this cause they couldn’t believe, for Isaiah said again:
Hivyo hawakuweza kuamini, kwani Isaya tena alisema:
40 “He has blinded their eyes and he hardened their heart, lest they should see with their eyes, and perceive with their heart, and would turn, and I would heal them.”
“Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya.”
41 Isaiah said these things when he saw his glory, and spoke of him.
Isaya alisema maneno haya kwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasema habari zake.
42 Nevertheless, even many of the rulers believed in him, but because of the Pharisees they didn’t confess it, so that they wouldn’t be put out of the synagogue,
Hata hivyo, wengi wa viongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuogopa kwamba watatengwa na sunagogi.
43 for they loved men’s praise more than God’s praise.
Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu
44 Jesus cried out and said, “Whoever believes in me, believes not in me, but in him who sent me.
Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, “Mtu aliyeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma.
45 He who sees me sees him who sent me.
Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma.
46 I have come as a light into the world, that whoever believes in me may not remain in the darkness.
Mimi ni mwanga, nami nimekuja ulimwenguni ili wote wanaoniamini wasibaki gizani.
47 If anyone listens to my sayings and doesn’t believe, I don’t judge him. For I came not to judge the world, but to save the world.
Anayeyasikia maneno yangu lakini hayashiki mimi sitamhukumu; maana sikuja kuhukumu ulimwengu bali kuuokoa.
48 He who rejects me, and doesn’t receive my sayings, has one who judges him. The word that I spoke will judge him in the last day.
Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.
49 For I spoke not from myself, but the Father who sent me gave me a commandment, what I should say and what I should speak.
Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila Baba aliyenituma ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini.
50 I know that his commandment is eternal life. The things therefore which I speak, even as the Father has said to me, so I speak.” (aiōnios g166)
Nami najua kuwa amri yake huleta uzima wa milele. Basi, mimi nasema tu yale Baba aliyoniagiza niyaseme.” (aiōnios g166)

< John 12 >