< John 7 >

1 After these things Jesus walked in Galilee: for he would not walk in Jewry, because the Jews sought to kill him.
Baada ya hayo, Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya. Hakutaka kutembea mkoani Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi walikuwa wanataka kumwua.
2 Now the Jews’ feast of tabernacles was at hand.
Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
3 His brethren therefore said unto him, Depart hence, and go into Judæa, that thy disciples also may see the works that thou doest.
Basi ndugu zake wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.
4 For [there is] no man [that] doeth any thing in secret, and he himself seeketh to be known openly. If thou do these things, shew thyself to the world.
Mtu hafanyi mambo kwa siri kama anataka kujulikana kwa watu. Maadam unafanya mambo haya, basi, jidhihirishe kwa ulimwengu.”
5 For neither did his brethren believe in him.
(Hata ndugu zake hawakumwamini!)
6 Then Jesus said unto them, My time is not yet come: but your time is alway ready.
Basi, Yesu akawaambia, “Wakati wangu ufaao haujafika bado. Lakini kwenu ninyi kila wakati unafaa.
7 The world cannot hate you; but me it hateth, because I testify of it, that the works thereof are evil.
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini mimi wanichukia kwa sababu mimi nauambia wazi kwamba matendo yake ni maovu.
8 Go ye up unto this feast: I go not up yet unto this feast; for my time is not yet full come.
Ninyi nendeni kwenye sikukuu hiyo. Mimi siendi kwenye sikukuu hiyo, maana saa yangu ifaayo haijafika.”
9 When he had said these words unto them, he abode [still] in Galilee.
Alisema hayo kisha akabaki huko Galilaya.
10 But when his brethren were gone up, then went he also up unto the feast, not openly, but as it were in secret.
Baada ya ndugu zake kwenda kwenye sikukuu, Yesu naye alikwenda, lakini hakuenda kwa hadhara bali kwa siri.
11 Then the Jews sought him at the feast, and said, Where is he?
Viongozi wa Wayahudi walikuwa wanamtafuta kwenye sikukuu hiyo; Wakauliza: “Yuko wapi?”
12 And there was much murmuring among the people concerning him: for some said, He is a good man: others said, Nay; but he deceiveth the people.
Kulikuwa na minong'ono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.”
13 Howbeit no man spake openly of him for fear of the Jews.
Hata hivyo hakuna mtu aliyethubutu kusema, habari zake hadharani kwa kuwaogopa viongozi wa Wayahudi.
14 Now about the midst of the feast Jesus went up into the temple, and taught.
Sikukuu hiyo ilipofikia katikati, Yesu naye alikwenda Hekaluni, akaanza kufundisha.
15 And the Jews marvelled, saying, How knoweth this man letters, having never learned?
Basi, Wayahudi wakashangaa na kusema “Mtu huyu amepataje elimu naye hakusoma shuleni?”
16 Jesus answered them, and said, My doctrine is not mine, but his that sent me.
Hapo Yesu akawajibu, “Mafundisho ninayofundisha si yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.
17 If any man will do his will, he shall know of the doctrine, whether it be of God, or [whether] I speak of myself.
Mtu anayependa kufanya yale anayotaka Mungu, atajua kama mafundisho yangu yametoka kwa Mungu, au mimi najisemea tu mwenyewe.
18 He that speaketh of himself seeketh his own glory: but he that seeketh his glory that sent him, the same is true, and no unrighteousness is in him.
Yeye anayejisemea tu mwenyewe anatafuta sifa yake mwenyewe; lakini anayetafuta sifa ya yule aliyemtuma, huyo ni mwaminifu, na ndani yake hamna uovu wowote.
19 Did not Moses give you the law, and [yet] none of you keepeth the law? Why go ye about to kill me?
Je, Mose hakuwapeni Sheria? Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishika Sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”
20 The people answered and said, Thou hast a devil: who goeth about to kill thee?
Hapo watu wakamjibu, “Una wazimu wewe! Nani anataka kukuua?”
21 Jesus answered and said unto them, I have done one work, and ye all marvel.
Yesu akawajibu, “Kuna jambo moja nililofanya, nanyi mnalistaajabia.
22 Moses therefore gave unto you circumcision; (not because it is of Moses, but of the fathers; ) and ye on the sabbath day circumcise a man.
Mose aliwapeni ile desturi ya kutahiri. (Si kwamba desturi hiyo ilitoka kwa Mose, bali ilitoka kwa mababu). Sasa ninyi humtahiri mtu hata siku ya Sabato.
23 If a man on the sabbath day receive circumcision, that the law of Moses should not be broken; are ye angry at me, because I have made a man every whit whole on the sabbath day?
Ikiwa basi, mtu hutahiriwa hata siku ya Sabato kusudi Sheria ya Mose isivunjwe, mbona mnanikasirikia kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya Sabato?
24 Judge not according to the appearance, but judge righteous judgment.
Msihukumu mambo kwa nje tu; toeni hukumu ya haki.”
25 Then said some of them of Jerusalem, Is not this he, whom they seek to kill?
Baadhi ya watu wa Yerusalemu walisema, “Je, yule mtu wanayemtafuta wamuue si huyu?
26 But, lo, he speaketh boldly, and they say nothing unto him. Do the rulers know indeed that this is the very Christ?
Tazameni sasa! Anawaonya hadharani, wala hakuna mtu anayemwambia hata neno. Je, yawezekana kuwa viongozi wametambua kweli kwamba huyu ndiye Kristo?
27 Howbeit we know this man whence he is: but when Christ cometh, no man knoweth whence he is.
Kristo atakapokuja hakuna mtu atakayejua mahali alikotoka, lakini sisi tunajua alikotoka mtu huyu!”
28 Then cried Jesus in the temple as he taught, saying, Ye both know me, and ye know whence I am: and I am not come of myself, but he that sent me is true, whom ye know not.
Basi, Yesu alipokuwa anafundisha Hekaluni alipaaza sauti na kusema, “Ati mnanijua; hata nilikotoka mnakujua! Hata hivyo, sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe; ila yeye aliyenituma mimi ni wa kweli, nanyi hamumjui.
29 But I know him: for I am from him, and he hath sent me.
Lakini mimi namjua kwa sababu nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.”
30 Then they sought to take him: but no man laid hands on him, because his hour was not yet come.
Basi, watu wakataka kumtia nguvuni, lakini hakuna mtu aliyethubutu kumkamata kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
31 And many of the people believed on him, and said, When Christ cometh, will he do more miracles than these which this [man] hath done?
Wengi katika ule umati wa watu walimwamini, wakasema, “Je, Kristo akija atafanya ishara kubwa zaidi kuliko alizozifanya huyu?”
32 The Pharisees heard that the people murmured such things concerning him; and the Pharisees and the chief priests sent officers to take him.
Mafarisayo waliwasikia watu wakinong'ona maneno hayo juu ya Yesu. Basi, wao pamoja na makuhani wakuu wakawatuma walinzi wamtie nguvuni.
33 Then said Jesus unto them, Yet a little while am I with you, and [then] I go unto him that sent me.
Yesu akasema, “Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kisha nitamwendea yule aliyenituma.
34 Ye shall seek me, and shall not find [me]: and where I am, [thither] ye cannot come.
Mtanitafuta lakini hamtaniona, maana pale nitakapokuwa ninyi hamwezi kufika.”
35 Then said the Jews among themselves, Whither will he go, that we shall not find him? will he go unto the dispersed among the Gentiles, and teach the Gentiles?
Viongozi wa Wayahudi wakasema wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi ambapo hatutaweza kumpata? Atakwenda kwa Wayahudi waliotawanyika kati ya Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki?
36 What [manner of] saying is this that he said, Ye shall seek me, and shall not find [me]: and where I am, [thither] ye cannot come?
Ana maana gani anaposema: Mtanitafuta lakini hamtanipata, na mahali nitakapokuwa ninyi hamwezi kufika?”
37 In the last day, that great [day] of the feast, Jesus stood and cried, saying, If any man thirst, let him come unto me, and drink.
Siku ya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalum. Yesu alisimama, akasema kwa sauti kubwa, “Aliye na kiu na aje kwangu anywe.
38 He that believeth on me, as the scripture hath said, out of his belly shall flow rivers of living water.
Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: Anayeniamini mimi, mito ya maji yenye uzima itatiririka kutoka moyoni mwake!”
39 (But this spake he of the Spirit, which they that believe on him should receive: for the Holy Ghost was not yet [given]; because that Jesus was not yet glorified.)
(Alisema hayo kumhusu Roho ambaye wale waliomwamini yeye watampokea. Wakati huo Roho alikuwa hajafika kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.)
40 Many of the people therefore, when they heard this saying, said, Of a truth this is the Prophet.
Baadhi ya watu katika ule umati walisikia maneno hayo, wakasema, “Kweli mtu huyu ndiye yule nabii!”
41 Others said, This is the Christ. But some said, Shall Christ come out of Galilee?
Wengine wakasema, “Huyu ndiye Kristo!” Lakini wengine walisema, “Je, yawezekana Kristo akatoka Galilaya?
42 Hath not the scripture said, That Christ cometh of the seed of David, and out of the town of Bethlehem, where David was?
Maandiko Matakatifu yasemaje? Yanasema: Kristo atatoka katika ukoo wa Daudi, na atazaliwa Bethlehemu, mji wa Daudi!”
43 So there was a division among the people because of him.
Basi, kukatokea mafarakano juu yake katika ule umati wa watu.
44 And some of them would have taken him; but no man laid hands on him.
Baadhi ya watu walitaka kumtia nguvuni lakini hakuna aliyejaribu kumkamata.
45 Then came the officers to the chief priests and Pharisees; and they said unto them, Why have ye not brought him?
Kisha wale walinzi wakarudi kwa makuhani wakuu na Mafarisayo; nao wakawauliza, “Kwa nini hamkumleta?”
46 The officers answered, Never man spake like this man.
Walinzi wakawajibu, “Hakuna mtu aliyepata kamwe kusema kama asemavyo mtu huyu!”
47 Then answered them the Pharisees, Are ye also deceived?
Mafarisayo wakawauliza, “Je, nanyi pia mmedanganyika?
48 Have any of the rulers or of the Pharisees believed on him?
Je, mmekwisha mwona hata mmoja wa viongozi wa watu, au mmoja wa Mafarisayo aliyemwamini?
49 But this people who knoweth not the law are cursed.
Lakini umati huu haujui Sheria ya Mose; umelaaniwa!”
50 Nicodemus saith unto them, (he that came to Jesus by night, being one of them, )
Mmoja wao alikuwa Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu. Basi, yeye akawaambia,
51 Doth our law judge [any] man, before it hear him, and know what he doeth?
“Je, Sheria yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza na kujua anafanya nini?”
52 They answered and said unto him, Art thou also of Galilee? Search, and look: for out of Galilee ariseth no prophet.
Nao wakamjibu, “Je, wewe pia umetoka Galilaya? Haya, kayachunguze Maandiko Matakatifu nawe utaona kwamba Galilaya hakutoki kamwe nabii!”
53 And every man went unto his own house.
Basi, wote wakaondoka, kila mtu akaenda zake;

< John 7 >