< 2 Petrova 3 >

1 Ljubljeni, pišem evo već drugu poslanicu. U objema opomenom budim vaš zdrav razbor
Wapenzi wangu, hii ni barua ya pili ninayowaandikia. Katika barua hizo mbili nimejaribu kufufua fikira safi akilini mwenu kwa kuwakumbusheni mambo haya.
2 da se sjetite riječi što ih prorekoše sveti proroci i zapovijedi apostola vaših, zapovijedi Gospodinove i Spasiteljeve.
Napenda mkumbuke maneno yaliyosemwa na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi mliyopewa na mitume wenu.
3 Znajte ponajprije ovo: u posljednje će se dane pojaviti podrugljivi izrugivači; povoditi će se za svojim požudama
Awali ya yote jueni kwamba siku za mwisho watakuja watu ambao mienendo yao inatawaliwa na tamaa zao mbaya. Watawadhihaki ninyi
4 i pitati: “Što je s obećanjem njegova Dolaska? Jer i otkad Oci pomriješe, sve ostaje kao što bijaše od početka stvorenja.”
na kusema: “Aliahidi kwamba atakuja! Je, sasa yuko wapi? Mambo ni yaleyale tangu babu zetu walipokufa; hali ya vitu ni ileile kama ilivyokuwa mwanzo wa ulimwengu!”
5 Ta oni naumice zaboravljaju da nebesa bijahu odavna i da zemlja na Božju riječ posta iz vode i po vodi.
Watu hao, kwa makusudi, husahau kwamba zamani Mungu alinena, nazo mbingu na nchi zikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika maji na kwa maji;
6 Na isti način ondašnji svijet propade vodom potopljen.
na kwa maji hayo, yaani yale maji ya gharika kuu, dunia ya wakati ule iliangamizwa.
7 A sadašnja nebesa i zemlja istom su riječju pohranjena za oganj i čuvaju se za Dan suda i propasti bezbožnih ljudi.
Lakini mbingu na nchi za sasa zahifadhiwa kwa neno la Mungu kwa ajili ya kuharibiwa kwa moto. Zimewekwa kwa ajili ya Siku ile ambapo watu wasiomcha Mungu watahukumiwa na kuangamizwa.
8 Jedno, ljubljeni, ne smetnite s uma: jedan je dan kod Gospodina kao tisuću godina, a tisuću godina kao jedan dan.
Lakini, wapenzi wangu, msisahau kitu kimoja! Mbele ya Bwana, hakuna tofauti kati ya siku moja na miaka elfu; kwake yote ni mamoja.
9 Ne kasni Gospodin ispuniti obećanje, kako ga neki sporim smatraju, nego je strpljiv prema vama jer neće da tko propadne, nego hoće da svi prispiju k obraćenju.
Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu.
10 Kao tat će doći Dan Gospodnji u koji će nebesa trijeskom uminuti, počela se, užarena, raspasti, a zemlja i djela na njoj razotkriti.
Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake.
11 Kad se sve tako ima raspasti, kako li treba da se svi vi ističete u svetu življenju i pobožnosti
Maadamu kila kitu kitaharibiwa namna hiyo, je, ninyi mnapaswa kuwa watu wa namna gani? Mnapaswa kuishi kitakatifu na kumcha Mungu,
12 iščekujući i pospješujući dolazak Dana Božjega u koji će se nebesa, zapaljena, raspasti i počela, užarena, rastaliti.
mkiingojea Siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi—Siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto.
13 Ta po obećanju njegovu iščekujemo nova nebesa i zemlju novu, gdje pravednost prebiva.
Lakini sisi, kufuatana na ahadi yake, twangojea mbingu mpya na dunia mpya ambayo imejaa uadilifu.
14 Zato, ljubljeni, dok to iščekujete, uznastojte da mu budete neokaljani i besprijekorni, u miru.
Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwa mnangojea Siku ile, fanyeni bidii kuwa safi kabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa na amani naye.
15 A strpljivost Gospodina našega spasenjem smatrajte, kako vam i ljubljeni brat naš Pavao napisa po mudrosti koja mu je dana.
Mnapaswa kuuona uvumilivu wa Bwana kuwa ni nafasi anayowapeni mpate kuokolewa, kama Paulo ndugu yetu mpenzi alivyowaandikia akitumia hekima aliyopewa na Mungu.
16 Tako u svim poslanicama gdje o tome govori. U njima ima ponešto nerazumljivo, što neupućeni i nepostojani iskrivljuju, kao i ostala Pisma - sebi na propast.
Hayo ndiyo asemayo katika barua zake zote anapozungumzia suala hilo. Yapo mambo kadhaa katika barua zake yaliyo magumu kuyaelewa, mambo ambayo watu wajinga, wasio na msimamo, huyapotosha kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko Matakatifu. Hivyo wanasababisha maangamizi yao wenyewe.
17 Vi dakle, ljubljeni pošto ste upozoreni, čuvajte se da ne biste, zavedeni bludnjom razularenika, otpali od svoje postojanosti.
Lakini ninyi, wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili. Basi, muwe na tahadhari msije mkapotoshwa na makosa ya waasi, mkaanguka kutoka katika msimamo wenu imara.
18 A rastite u milosti i spoznanju Gospodina našega i Spasitelja Isusa Krista! Njemu slava i sada i do u dan vječnosti! Amen! (aiōn g165)
Lakini endeleeni kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu uwe kwake, sasa na hata milele! Amina. (aiōn g165)

< 2 Petrova 3 >

The World is Destroyed by Water
The World is Destroyed by Water